AHMED Ally, Kaimu Kocha wa timu ya KMC amesema kuwa kikubwa ambacho kwa sasa wanakifanya ni kuandaa kikosi chenye ushindani kitakachowapa matokeo chanya kwenye mechi zao zote.
KMC inajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Novemba 22 mkoani Mwanza dhidi ya Alliance uwanja wa Nyamagana.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ally amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo jambo linalowafanya wapambane kujiweka sawa.
"Mechi ni nyingi na kila timu imejipanga kupata matokeo, tupo vizuri na tutafanya vema kwenye mechi zetu za ushindani.
"Ligi ina ushindani mkubwa nasi tupo tayari kwa ushindani jambo ambalo linatufanya tujipange kwa kila mechi inayofuata," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment