November 30, 2019


Imefahamika kuwa wakati wowote Klabu ya Simba itaachana na benchi zima la ufundi huku tetesi zikimtaja kocha wa sasa wa Polisi Tanzania, Suleiman Matola anaweza kurejea ‘nyumbani’ kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

Hiyo imekuja ikiwa ni saa chache kabla ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo ikitarajiwa kukutana jana usiku na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kuzungumzia hatima yake kwenye timu hiyo iliyo chini ya Denis Kitambi hivi sasa.

Ni mara ya pili mfululizo kwa Matola kutajwa kwenye misimu miwili ya hivi karibuni, awali ilikuwa kwenye msimu uliopita kabla ya Kitambi kupewa nafasi hiyo ya kocha msaidizi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kutoka ndani ya bodi ya timu hiyo muda wowote klabu hiyo itatangaza kuachana na benchi zima la ufundi.

2 COMMENTS:

  1. Mtuambie ukweli kama mnamfukuza ama ni vipi na mnamfukuza kwa kosa gani? Mbona hamueleweki?

    ReplyDelete
  2. 1. Kuondoka kwenye kituo Cha kazi kwenda Afrika kusini bila ruhusa ya muajiri hapa tukumbuke yeye mwenyewe anakili aliomba alitoa taatifa kwa E-mail Kisha akaondoka hakusubili jibu 2. Lukataa wito halali wa Viongozi kwenda kuongelea mtafaruku aliosababisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic