November 13, 2019


Baada ya kusakamwa mitandaoni juu ya kauli yake kuhusiana na alichomweleza kipa wa Simba, Aishi Manula, Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Juma Mgunda, amefunguka juu ya alichokisema.

Mgunda ameeleza kuwa alichokieleza kuhusu Aishi Manula wengi wamechukua neno moja badala ya sentesi nzima.

Juzi Mgunda aliibuka na kusema kuwa Manula hakuitwa Stars sababu wao kama makocha hawaendi kupeleka posa na badala yake wanaangalia wachezaji stahiki.

"Naomba nitoe msisitizo kwamba taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilininukuu vibaya na kilichofanyika ni kwamba lilichukuliwa neno moja na sio sentensi nzima."

"Mimi nilieleza kuwa wachezaji waliochaguliwa kwa kipindi hiki ndiyo wachezaji wanaofaa kwa kuzingatia hali halisi ilivyo kwa sasa.

"Malinda mlango wa Simba Aishi Manula wakati wake ukifika tena ataendelea kutumika timu ya Taifa Stars."

6 COMMENTS:

  1. sasa ungesema maneno hayo tu pangekuwa na tatizo, shida umeweka taarabu nyingi kwamtu anaependwa na wengi, angalia kisije ota nyasi.

    ReplyDelete
  2. Ukweli kwamba ujue manula kiwango kimeshuka cha kudKa katika tmu y taifa ilo utambue

    ReplyDelete
  3. kwani bila manula hakuna taifa stars.....by the way soksi alizovaa zimempendeza sana

    ReplyDelete
  4. mnaleta ushabiki wenu wa Yanga kwenye masuala ya msingi ishu so manula ishu kauli ya kocha inaonyesha kabisa ana chuki na mchezaji husika au kuna msukumo nyuma yake kuhusu kutoitwa kwa Manula

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic