November 13, 2019


PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wataendelea kujinoa kwa sasa licha ya kuwa na wachezaji wachache ambao wamebaki kwenye kikosi chake.

Aussems amesema kuwa mazoezi kwa wachezaji wake ni muhimu katika kujenga uimara wa kikosi chake kwenye ligi ambayo ina ushindani.

"Kuna ushindani mkubwa wa ligi kwa sasa na kila mmoja anapambana kufanya vema, licha ya wachezaji wangu baadhi yao kuitwa timu ya taifa bado tutaendelea na maandalizi.

"Kuitwa kwao timu ya Taifa ni jambo jema na inamaanisha kwamba kuna kitu ambacho kipo kwao hivyo tutaendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi za ligi," amesema.

Miongoni mwa nyota ambao wameitwa kwenye timu za taifa ni pamoja na Miraj Athuman, 'Sheva', Mohamed Hussein 'Tshabalala', Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga hawa wapo timu ya taifa ya Tanzania huku Shiboub akiitwa timu ya Taifa ya Sudan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic