November 17, 2019


KOCHA Mkuu wa klabu ya Inter Milan, Antonio Conte amepokea barua iliyoambatanishwa na risasi pamoja na ujumbe wa vitisho kutoka kwa mtu asiyejulikana kwa mujibu wa ripoti kutoka ndani ya Italia.

Ripoti zinaeleza kuwa ujumbe huo alipewa kocha huyo anayekinoa kikosi cha Inter Milan umeacha hali ya wasiwasi ndani ya klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Italia jambo lililofanya wamuongezee ulinzi kwa muda ili kumuepeusha na hatari hiyo.

Polisi wamesema kuwa wapo kwenye uchunguzi wa kina ili kupata majibu ya ujumbe huo wa vitisho kwa kuchunguza alama za vidole ili kutambua utambulisho wa mtu huyo asiyejulikana ambaye anayemtisha kocha huyo wa zamani wa Chelsea pamoja na Juventus.

Conte ameanza kujilinda yeye mwenyewe na familia yake baada ya kupokea ujumbe huo kwa kuwa na walinzi nyumbani na wengine kuwa nao anapokuwa na timu wakati akitoa mafunzo kwa timu yake huku mabosi wake wakisema kuwa wamepatwa na mshtuko kuhusu jambo hilo.
Inter ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 31 ndani ya Serie A ikiwa imecheza jumla ya mechi 12 imeshinda 10 na kupata sare moja na imepoteza mchezo mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic