MKWASA WALA HANA TATIZO NA MOLINGA, AZUNGUMZIA UZITO WAKE
Kocha ambaye Wazungu kibao wanaitamani nafasi yake Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema hana shida na uzito wa David Molinga.
Mkwasa alisema kila mchezaji wa kikosi hicho anayo nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza kama ataonyesha kujituma, hivyo Molinga naye atacheza kwenye kila mchezo kama ataonyesha juhudi ya kufunga mabao kwenye mazoezi ya timu hiyo na kwemye michezo ambayo atakuwa anacheza.
“Sina shida na uzito au unene wa Molinga ninachokihitaji mimi nikumuona akitimiza majukumu yake ya kufunga na kuonyesha juhudi kwenye mazoezi.
"Siyo yeye tu kila mchezaji anayo nafasi ya kucheza Yanga endapo atatimiza majukumu yake uwanjani na kwenye mazoezi ya timu.” amesema Mkwasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment