November 9, 2019


JACKSON Mayanja aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC amepigwa chini mazima ndani ya klabu yake ya KMC kutokana na kuwa na kile kilichoelezwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Mayanja ambaye aliwahi kuinoa Simba alipewa kandarasi ya mwaka mmoja na KMC ambayo iliachana na Kocha wao Etienne Ndayiragije aliyetua Azam FC kabla ya kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars.

Akizungumza na Saleh Jembe Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa wamekubaliana na Mayanja kiusawa kutokana na mkataba wake ulivyokuwa ukimwelekeza.

"Mayanja ni mwalimu mzuri ila kutokana na makubaliano yetu kwa pamoja tumeona ni bora aendelee na maisha yake na kwa sasa hayupo Bongo alikuwa ana matatizo ya kifamilia," amesema.

Mayanja anakuwa ni kocha wa tatu kupigwa chini baada ya Bilo wa Alliance, Zahera wa Yanga kumtangulia.

2 COMMENTS:

  1. Naona dalili za Aussems za kuwafuata kina Zahera, Mayanja zimewadia maana dalili za mvua ni mawingu.Timu inapoamua kuajiri kocha wa kigeni ina maana ana vitu special na mbinu za ziada ukilinganisha na makocha wetu wazawa ambao hata leseni walizonazo hazieleweki.Mimi kama mdau wa soka na mwanachama wa Simba nimefuatilia mechi zote za Simba alizocheza za klabu bingwa Africa (UD Songo), ligi yetu (mechi tisa) na za kirafiki(Bandari,Mashujaa, Aigre Noire)tokea mwezi July hadi sasa lakini nimebaki na maswali ambayo nashindwa kuyajibu.Mechi karibia zote Simba walizocheza wanamiliki mpira kwa asilimia kubwa sana kuliko wapinzani ukitoa mechi waliyocheza na Azam ambao walimiliki mpira zaidi ya Simba.Inakuwaje timu yako wakati wote inauchezea mpira tu bila kufunga magoli mengi? mpira ni magoli na ili upate pointi tatu inabidi ushinde mechi na siyo kumiliki mpira tu.Hii wadau wenzangu wa Simba imekaaje kwa klabu kuwa na kocha mwenye leseni daraja A tena ya UEFA na ashindwa mbinu na makocha wazawa wenye leseni hata hazieleweki.Mechi iliyonistua zaidi ni hii ya Prison ya kwenda suluhu kwenye uwanja usiokuwa na matuta wala mabonde na vipi wakikutana uwanja wa sokoine mbeya? kocha ataendelea kutuaminisha kuwa uwanja ni mbovu ndio maana hapati matokeo mazuri kama alivyo lalamikia viwanja vya Lake Tanganyika(Kigoma), Karume (Musoma) au Amri Abeid (Arusha) shinyanga stadium? Bodi ya wakurugenzi wa Simba naelewa mnajitahidi sana kutimiza wajibu wenu ili kufanikisha maendeleo ya klabu yetu lkn tuanze kuweka jicho la tatu na mwenendo wa timu yetu kuhusu perfomance na matokeo tunayopata.Wachezaji karibia wote wa Simba ni wazuri na ninaamini kuwa hata wakienda timu zingine za ligi kuu wataingia first eleven na masilahi wanapata ya kuridhisha kuliko timu zingine lkn mwenendo wa timu unatia mashaka na tusipochukua tahadhari kurekebisha pale tunaona sivyo tusije kushangaa yaliyo tukuta walicho tufanyia Green warriors na Mashujaa.Ni vyema tuangalie na kutathimini graph ya matokeo ya timu kwa mechi zote Simba imecheza tokea July pre-season hadi sasa.Tusijipe moyo wa kuwa "tumpe muda kocha" kila baada ya mechi ama sivyo chelewa-chelewa utakuta mwana si wako.Nawasilisha hoja hasa kwa wadau wenzangu wa Simba.

    ReplyDelete
  2. Wacha fitna na ushamba. Aussems yuko vzuri. Hata barcelona, man city, real madrid, bayern munich, PSG na wengine nao wanapoteza mechi, sembuse simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic