November 9, 2019


Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya KMC upo kwenye mazungumzo na makocha Masoud Djuma pamoja na Joseph Omogo waliowahi kuinoa Simba.

Imeelezwa kuwa maamuzi hayo yanakuja kutokana na klabu hiyo kumtimua kazi kocha Mganda, Jackson Mayanja kufuatia kuwa na mwenendo mbaya wa matokeo ndani ya timu.

Omog ambaye ni raia wa Cameroon, anatajwa kuchukua nafasi ya Mayanja sambamba na Masoud ambaye ni raia wa Burundi.

Kuna uwezekano makocha hao wawili wanaweza kuwa sehemu ya timu ya KMC na muda wowote kuanzia sasa wanaweza wakatangazwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic