November 3, 2019


Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa mabosi wa Simba walimsajili winga kutoka TP Mazmbe, Deo Kanda kutokana na historia yake ya mpira.

Zahera ameeleza licha ya usajili huo kufanyika, Kanda alikuwa na matatizo ndani ya Mazembe kitu ambacho anaamini kilimpa urahisi kuondoka pale.

Zahera amefunguka kwamba Kanda alikuwa hapatai nafasi ndani ya kikosi cha TP Mazembe hivyo ikawa ni urahisi kwa Simba kupata saini yake.

“Soka la Afrika lina tatizo, unajua Simba nani alienda kumuona Deo Kanda akicheza?

Jibu hakuna, ila ukweli alikuwa na shida na timu yake TP Mazembe, hakuwa anacheza ligi lakini Simba wakamsajili.

“Huwezi sema Simba walikosea kwa kuwa Kanda ni mchezaji mzuri na wamemchukua kutokana na historia yake."

10 COMMENTS:

  1. akisema ukweli anaambiwa chizi

    ReplyDelete
  2. Zungumzia timu yetu.Simba nä wachezaji wake hayatuhusu.Umesikia kocha wa Simba akizungumzia wachezaji wa Yanga???

    ReplyDelete
  3. Huyu kocha wetu ni kioja. Amesema eti hakumpanga Balinya kwa sababu wapenzi wa Yanga walimzomea Balinya kwenye mchezo dhidi ya Polisi. Kwa hiyo akasema kama walimzomea yeye Zahera ampange kwa nini?Kweli safari hii tumepata kocha!!!

    ReplyDelete
  4. Mbona Manara yupo na Yanga kuanzia Mwanza mpaka Cairo na hamsemi aiache Yanga haimhusu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Manara ni mmoja wa mashabiki wa Yanga na chimbuko la wazazi wake ni pale. Ni lazima aepende timu iliyomkuza

      Delete
    2. kweli chizi so mpaka aokote makopo hv kwenda kuangalia mechi ya yanga basi kashakua anaipenda yanga nyie mnajisikiaje kuwa na mshabiki anayewakejeli na kuisifia simba kila uchao

      Delete
  5. Inamuhusu nini huyo mkongo zungumzia hao kandambili wako

    ReplyDelete
  6. Hyu mtu anawashwa washwa na Simba, haongei ya kwake tu mpaka aitaje Simba..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic