MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hakuna raha yoyote anayoipata kufunga mabao yake kwani anakamiwa na wapinzani mwanzo mwisho akiwa ndani ya uwanja.
Kagere ni kinara wa kutupia ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ametupia jumla ya mabao 8 mpaka sasa kwenye mechi 8 ambazo Simba imecheza.
Kagere amesema: "Hakuna raha kwenye kufunga kwani ninapitia magumu mengi ikiwa ni safu ya mabeki ambao kwa sasa wananitazama kwa ukaribu, nafurahi kuona namna ninavyofunga kwa ajili ya timu hivyo siangalii idadi ya mabao bali naangalia ushindi tunaopata.
"Suala la kufunga mabao sio langu peke yangu ni kwa kila mchezaji ndio maaana tunacheza tukiwa timu, kitu kikubwa kwetu ni ushindi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment