NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Granit Xhaka, amesema ameanza kutafuta nyumba ya kuishi nchini Italia.
Hatua hiyo imekuja huku tetesi za yeye kuhusishwa kuhamia AC Milan ya nchini humo zikizidi kushika kasi.
Katika usajili wa Januari, mwakani, Xhaka anatarajiwa kuondoka Arsenal, hii ni baada ya sakata lililomkumba la kuvuliwa unahodha kutokana na mgogoro wake na mashabiki.
Mtendaji Mkuu wa AC Milan, Ivan Gazidis ambaye aliwahi kufanya kazi Arsenal, ndiye aliyechangia kiungo huyo asajiliwe kikosini hapo mwaka 2016 na hivi sasa inaweza kuwa rahisi kumchukua tena.
0 COMMENTS:
Post a Comment