November 14, 2019


Simba, Yanga SC Martha Mboma, Dar es Salaam KLABU ya Lipuli, imeweka rekodi kwa mara ya kwanza kuwa timu ambayo imefunga mabao mengi zaidi ya Simba na Yanga katika Ligi Kuu Bara.

Lipuli imefunga mabao 18 katika mechi 10 ambazo imecheza hadi sasa msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara inayoshirikisha timu 20.

Timu hiyo kwenye mechi 10 ambazo imecheza, mechi tano imeshinda na kupoteza mbili tu, huku ikitoa sare tatu na kujikusanyia pointi 18. Kwenye msimamo inashika nafasi ya tatu nyuma ya vinara Simba na Kagera Sugar wanaoshika nafasi ya pili.

Simba ambayo mshambuliaji wake Meddie Kagere anaongoza kwa kufunga mabao akiwa nayo nane, yenyewe imefunga mabao 16 katika mechi tisa, huku Yanga ikifunga mabao sita katika mechi tano.

Kwa maana hiyo, Lipuli imeifunika Simba na Yanga ambazo ndizo zinaaminika kuwa na washambuliaji hatari zaidi na mara kadhaa wamekuwa wakiongoza kwa ufungaji. Ingawa ni mwanzoni tu mwa ligi lakini ni picha kuwa huko mbele mambo yatakuwa hatari zaidi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic