November 14, 2019


KLABU ya Simba, imesema kuwa, kabla ya kufanyika kwa mkutano wao mkuu, watakuwa tayari wameuzindua uwanja wao uliopo Bunju jijini Dar es Salaam.

Simba chini ya mwekezaji wake, Mohammed Dewji ‘Mo’, ulianza kujenga uwanja wao wa mazoezi ambapo awali ulitarajiwa kumalizika Februari, mwaka huu, lakini changamoto zilizojitokeza zikakwamisha ujenzi huo ambao sasa imetangazwa utakuwa sawa Desemba, mwaka huu.

Katibu wa Simba, Anold Kashembe, amesema kikubwa kinachokwamisha kukamilika kwa uwanja huo ni kutokana na mvua zisizoeleweka kuendelea kunyesha mara kwa mara.

“Kuna mvua ambayo imenyesha hapa kati ndiyo imetibua hasa katika ule uwanja wa nyasi bandia ambapo ule udongo umevurugika, lakini upande wa nyasi asilia mambo yanakwenda vizuri. “Kutokana na hilo, tarehe 7 ya mwezi ujao, kabla ya mkutano mkuu haujafanyika, tunatarajia kuuzindua rasmi uwanja wetu huu.

“Unajua tumekuwa tukitumia gharama nyingi sana sehemu ambayo tumekuwa tukienda kufanya mazoezi, hivyo tumeamua kuitengeneza pitch (sehemu ya kuchezea) haraka, kisha masuala ya hosteli na mengine yatafuata,” alisema Kashembe.

Desemba 8, mwaka huu, Klabu ya Simba inatarajiwa kufanya mkutano mkuu ambapo siku moja kabla ya mkutano huo, ndipo watauzindua uwanja wao.

1 COMMENTS:

  1. Hiyo ndio Simba bila ya malumbano inateleza mbele kimyakimya kama nyoka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic