BODI ya Madaktari wa timu ya Taifa ya Misri imethibitisha kuwa nyota wa Liverpool, Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 27 hali yake haijatengamaa.
Salah ana maumivu ya enka ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace hali iliyomlazimu aukose mchezo dhidi ya Manchester United.
Kiongozi wao Dr.Mohamed Abul-Ela amethibitisha kwamba bado Salah hajawa tayari kucheza mechi za ushindani kwa sasa.
Salah atakosa mchezo dhidi ya Kenya na Comoro ambayo ni maalumu kwa ajili ya michuano ya Afcon kwa kuwa anahitaji muda mrefu kurejea kwenye ubora.
"Mchezaji alikuja kambini Jumanne jioni akawa chini ya uangalizi hata alipokuwa akifanya mazoezi uwanja wa Burj Al Arab alikuwa kwenye uangalizi," ilieleza ripoti hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment