Kikosi cha Simba cha vijana jana kilipoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Soccer Net Academy kwa bao 1-0 uliochezwa katika uwanja wa Missionary mjini Morogoro.
Simba imekubali kupoteza mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Combine katika mechi iliyopita.
Licha ya kupoteza, Kocha wa kikosi hicho alisema vijawana wake walipambana lakini bahati haikuwa yao.
Aidha, Kocha huyo ameeleza watajitahidi kurekebisha makosa kadhaa yaliyojitokeza ili yasijirudie kuelekea mechi zijazo.
Baada ya kupoteza jana, kikosi hicho kitasafiri kuelekea wilayani Malinyi kwa ajili ya mechi zingine za kirafiki.
0 COMMENTS:
Post a Comment