SADIO Mane, mshambuliaji wa Liverpool amesema kuwa ataendelea kujirusha kwenye mechi ambazo atakuwa anacheza kwa ajili ya faida ya timu yake.
Mane amekuwa na tabia ya kujirusha akiwa ndani ya 18 mara anapoguswa na mchezaji wa timu pinzani jambo ambalo limemfanya meneja wa kikosi cha Manchester City. Pep Guardiola kumponda kwa tabia hiyo akidai ni bingwa wa kujirusha licha ya ubora wake.
Mane amesema :"Nitaendelea kujirusha kwa ajili ya manufaa ya timu yangu kwani ni ujanja tu unaofanywa niangaliwe zaidi kwa umakini nitaendelea kucheza kwa mtindo huo bila kujali wanaonisema." amesema.
Mane amesababisha penalti kwa timu yake kwenye mechi dhidi ya Leicester City na Tottenham mwezi uliopita pia aliwahi kuonyeshwa kadi ya njano mbele ya Aston Villa wiki iliyopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment