November 22, 2019


ABDALAH Mohamed 'Bares' kocha mkuu wa timu ya JKT Tanzania amesema kuwa kikosi chake kipo tayari Kwa mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema kuwa ugumu wa ligi umeikomaza timu jambo linalomfanya azipigie hesabu pointi tatu za Yanga kwa umakini.

"Hakuna ambaye haoni kwa sasa namna ushindani ulivyo, nimewapa majukumu wachezaji na wanatambua kwamba tunahitaji pointi tatu ili kuzidi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya ushindani.

"Tunatambua aina ya timu tunayokutana nayo ni ngumu na ina wachezaji wenye uzoefu hilo halitupi taabu kwani mpira ni dakika 90 tutapambana, mashabiki watupe sapoti," amesema.

JKT Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa imecheza mechi 10 na pointi zake 15 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya 15 imecheza mechi tano na ina pointi zake 10.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic