November 15, 2019


Mchezaji wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgossi ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Wanawake ya Simba (Simba Queens), jana alijjumuika na makocha wa timu ya wakubwa kufanya mazoezi.

Mazoezi hayo yalikuwa sehemu ya vitendo katika kozi ya CAF Diploma C ya Ukocha ambayo inaadaliwa na Shirikisho la Soka Afrika.

Mgosi amepata fursa hiyo kwa mara ya kwanza kujumuika katika mafunzo hayo, jambo ambalo linakuwa linaweka alama ya kumbukukumbu kwake na ndani ya kikosi cha Simba.

Baada ya mazoezi hayo, imeelezwa Mgosi amefurahia kuwa sehemu ya waliopata kozi hiyo kutokana na kumuongezea hadhi katika majukumu ya ukocha.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic