MISS Tanzania mwaka 2005 na pia mjasiriamali, Nancy Sumari, leo Novemba 27, 2019, amefanya ziara ndani ya kampuni ya Global Group alipokuja kutambulisha rasmi kitabu chake kwenye kipindi maalumu kilichorushwa na +255 Global Radio.
Katika mahojiano hayo kwenye kipindi maalumu, Nancy amesema;-“Ninayo furaha kubwa na ya kipekee kutangaza ujio wa kitabu changu cha pili cha watoto!
“Kitabu hiki, kinachoenda kwa jina la Haki, ni hadithi iliyotungwa kutokana na sheria ya haki za mtoto ya mwaka 2009, ili kuwasaidia watoto wa Tanzania kuzijua na kuzilinda haki zao.
“Karibuni, pametokea ongezeko la vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa haki za watoto kwa namna nyingi, zikiwemo mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, na mengine mengi yasiyofaa kwa maendeleo na ustawi wa watoto wetu.
“Kwa kupitia kitabu hiki cha Haki, ninatarajia kumfundisha mtoto wa Tanzania, kuzijua, kuzitambua na kuzilinda haki zake, na vilevile kuibua mjadala kati ya watoto, wazazi, walezi, jamii na taifa kwa ujumla, kuhusu haki za watoto.
“Kwa nafasi yake, anaweza kubeba jukumu la kuzisimamia pamoja na kuwalinda watoto wetu, katika Tanzania tunayoitaka.” Kitabu cha Haki kitapatikana:-TPH Bookshop – Dar es Salaam na Dodoma
A Novel Idea – Dar es Salaam na Arusha
Kase Book Store – Arusha
Kupitia namba ya simu – 0759344328 Kwa ajili ya kutumiwa popote ulipo.
0 COMMENTS:
Post a Comment