TIMU ya Yanga imeweka kambi tayari mkoani Mwanza leo kwa ajili ya kujiaandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaoatarajiwa kuchezwa Ijumaa, Novemba 29.
Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-2 mbele ya JKT Tanzania huku Alliance FC ikiwa na kumbukumbu ya kupteza kwa kufungwa mabao 5-0 dhidi ya Azam FC uwanja wa Nyamagana,
Charlse Mkwasa, Kocha wa Yanga amesema kuwa kikosi kipo sawa na morali ni kubwa kwa ajili ya mchezo huo muhimu.
"Mchezo wetu utakuwa mkubwa na mgumu hivyo tutawafuata wapinzani wetu tukiwa na tahadhari kubwa ili kupata matokeo chanya," amesema.
Mtazipata bila ya panic au maneno mengi kwakuwa timu hiyo ni dhaifu ni Jana Tu imechapwa mabao matano
ReplyDelete