KIKOSI cha
Simba leo kimelipa kisasi cha kupoteza mchezo wake mbele ya Mwadui FC kwa kufungwa bao 1-0 uwanja wa Kambarage kwa kuichapa mabao 4-0 Mbeya City. uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru.
Mchezo wa leo ulikuwa ni wa ushindani mkali ambapo iliwalazimu Simba kusubiri mpaka
dakika ya 8 kuandika bao la kwanza kupitia kwa Meddie Kagere ambaye alifunga
bao hilo kwa penalti baada ya Miaji Athuman kufanyiwa madhambi ndani ya eneo
la 18.
Kazi
haikuishia hapo zikiwa zimebaki dakika tatu kwenda muda wa mapumziko dakika ya
43 kiungo Clatous Chama alifunga bao la pili akiwa nje ya 18 akimalizia pasi ya
Ibrahim Ajibu mpira uliomshinda mlinda mlango wa Mbeya City na kuifanya Simba
kwenda vyumba vya mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha
pili Simba ilianza kwa kufanya mabadiliko kwa kumtoa Miraj ambaye nafasi yake
ilichukuliwa na Francis Kahata mambo yakazidi kuwa magumu kwa Simba ambapo
Mbeya City ilichangamka kutafuta mabao ya kusawazisha huku ikimtumia
mshambuliaji wao Peter Mapunda.
Iliawalizimu
Simba kusubiri mpaka dakika ya 78 kufunga bao la tatu kupitia kwa Sharaf Shiboub
aliyemalizia pasi ya Ajibu kabla ya dakika ya 83 Ajibu kumpisha Deo Kanda ambaye
alichukua dakika nne kuandika bao la nne akimalizia pasi ya Clatous Chama.
Ushindi huo
unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 21 baada ya kucheza mechi nane
imeshinda saba na imepoteza mechi moja huku Mbeya City ikiwa imeshinda mechi
moja kati ya tisa iliyocheza mpaka sasa na imetoa sare tano na kupoteza mechi
tatu.







THIS iS SIMBA tunawasubiri kandambili wapakatwe na waarabu usiku huu
ReplyDelete