DENIS Zakaria nyota anayekipiga kwenye klabu ya Borussia Mochengladbach inaelezwa kuwa ahatakuwa na timu hiyo wakati wa mwezi januari.
Wakala wa Zakaria, Mathieu Beda amesema kuwa amepata ofa nyingi zikitaka kupata saini ya nyota huyo mwenye makeke ndani ya uwanja.
"Sina uhakika kama Zakaria atabaki ndani ya Mochengladbach mwezi Januari kutokana na ofa ambazo zipo mkononi kwa sasa.
"Ana uwezo mkubwa na wengi wanatambua namna gani anavypambana kwa ajili ya timu yake, ninaamini kwa dili ambazo zipo hatadumu ndani ya timu yake kwa sasa," amesema.
Nyota huyo amecheza jumla ya mechi 11 amefunga mabao mawili na ana asisiti moja aliyotoa huku timu yake ikiwa namba moja na pointi zake 25 ndani a Bundesliga.
0 COMMENTS:
Post a Comment