ROJAS
Gabriel, beki wa kikosi cha Mwadui FC aliyesajiliwa msimu huu akitokea
Mtibwa Sugar amesema kuwa walipewa majukumu ya kuwabana washambuliaji wote wa
Simba wanaoongozwa na Meddie Kagere pamoja na Miraj Athuman mwanzo mwisho jambo
lililowafanya wasilete madhaara.
Simba ikiwa
inaongozwa na Kagere ilipoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu mbele ya Mwadui FC uwanja wa Kambarage baada ya kucheza mechi sita ambazo ni sawa na dakika 540
bila kupoteza .
Akizungumza
na Saleh Jembe, Rojas amesema kuwa walitumia muda mwingi kuisoma Simba
na falsafa yao jambo ambalo halikuwapa taabu kuwadhibiti kwenye mchezo wao wa
ligi.
“Tuliwatambua
ni washambuliaji wa aina gani hasa muda wao wa hatari ni ule wakiwa na mpira
mguuni na kabla ya kupokea mpira wanakuwa wanyumbulifu kutafuta nafasi jambo
hilo lilitufanya tuwachunge mwanzo mwisho.
“Hakukuwa na
nafasi ya Kagere wala alipoingia Miraji kuachwa kutembea peke yake kauli yetu
ilikuwa ni mtu na mtu mpaka mwisho wakachoka kutokana na kubwanwa na juhudi
zilitusaidia tukaibuka na pointi tatu,” amesema Rojas.
0 COMMENTS:
Post a Comment