November 29, 2019


Wakati Simba wakiwa katika harakati za kukamilisha ujenzi wa viwanja vyao vya mazoezi, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amewapiga kijembe kwa kueleza uwanja huo wamejengewa na Mohammed Dewji na si nguvu zao.

Mwakalebela ameibuka na kusema wao kama Yanga wameanza mchakato wa kujenga uwanja katika eneo walilokabidhiwa na serikali Kigamboni na akieleza wataujenga kwa nguvu zao wenyewe.

Kiongozi huyo amefunguka akisema kwa kushirikikiana na wananchi anaamini watapambana kwa kila namna ili kufanikisha zoezi hilo ambalo linachukua muda kukamilika

"Sisi tutajenga uwanja kwa nguvu zetu, hatushindani na Simba ambao wamejengewa uwanja na Mo Dewji.

"Tutajenga uwanja wa kisasa kwa nguvu za wanayanga wenyewee."

18 COMMENTS:

  1. Huyu Mwakalebela mbona kauli zake na CV take haviendani ? Namshauri akafanye Sanaa ya vichekesho maana ana kipaji tosha.

    ReplyDelete
  2. Mo Dewji kwani sio Simba mpaka unasema wamejengewa ( KIFUU TUNDU WEWE)

    ReplyDelete
  3. Kumbe mnao uwezo mkubwa wa hela na ikiwa ni Hivo kwanini mnamtesa Kwa kutomlipa Dante hela ya jasho lake na kumtaka eti akubali kulipwa kiduchuduchu. Muhofeni Mungu Kwa kumlipa haki zake pia kuwataka wengine wakuaminini na kuwaondoa hofu ili yasiwafike yaliyomfika Dante na wengineo

    ReplyDelete
  4. umaskini sio maradhi ukubali mwenzio akupe ushauri na wewe ufaidike,sasa unantukana mwenzako wakati yanga hata tofali bado hamjafyatua.

    ReplyDelete
  5. Kwani Uwanja wa Kaunda siyo wao?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  6. Mwakalebela na wenzie ni matapeli hapo wanatengeneza mipango ya kupiga pesa za michango ionekane wanataka kutujengea uwanja kumbe wababaifu wakubwa!hao mbwa wote wezi jamani

    ReplyDelete
  7. Kwa akili hiyo Yanga haina jengo kwani walijengewa na Marehemu Karume wakati Simba walijenga wenyewe. Mwakalebela wacha kujilinganisha na Simba.Sisi wanayanga tunataka kusikia viongozi mnafanya nini?Sio Simba wamefanya nini?

    ReplyDelete
  8. Huyu jamaa kwa maneno yake tuu anaonekana ni tapeli anatakiwa kutumbuliwa.

    ReplyDelete
  9. Uwanja wenyewe tumepewa na Makonda hatujanunua wenyewe .Kuliko kupiga domo kuhusu Simba tujaribu kujenga uwanja sasa. Mwakalebela wakati mwingine ni bora kukaa kimya kuliko kuonyesha upumbavu wako hadharani.

    ReplyDelete
  10. Kwa staili hii basic tutasubiri sana mabadiliko ndani ya klabu yetu Yanga.kutegemea nguvu ya wananchi pekee ni ndoto ya alinacha na kama tunajifanya vipofu Kwa wanayofanya watani zetu wa jadi basi kuna siku bakora zitatembea jangwani.Vijembe visivyo na tija ni ulimbukeni uliopitiliza.Tunahitaji mfumo wa mabadiliko ya kisasa ya kuendesha klabu.
    Mambo ya kuchangishana kama tuna sherehe za arusi na haina ukaguzi wa mahesabu ni utapeli tu.Pesa zimechangwa Kwa ajili ya usajili lkn kina Dante bado wanaidai klabu.leo Mwakalebela unataka kutuchangisha tena?Au ndio za kumlipa Zahera? Kumbukeni ahadi zenu kabla ya kuchaguliwa mlitoa ahadi ya mfumo wa mabadiliko au ndio kuteua kamati kila siku ndio mfumo wenyewe wa mabadiliko? Jitafakarini na sio kutoa vijembe ili kufurahisha wana Yanga.Wenzetu wanatuacha, wanasonga mbele hivyo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wa aina hii hawataki mabadiliko, wanatumia neno la wananchi kama kinga!

      Delete
  11. ubunge kachemsha hajapata,sasa na soka pia anataka kuchemka

    ReplyDelete
  12. Jiwe limerushwa gizani na tumesikia kelele zao hahahahahahahah

    ReplyDelete
  13. maneno ya mkosaji#simba nguvu moja.

    ReplyDelete
  14. Huyu kiongozi anasafiri na timu hana hata hela ya juisi!!

    ReplyDelete
  15. Wananchi wajenge uwanja, wamlipe Dante, wamlipe Zahera, January mkivunja mikataba na wachezaji wananchi walipe!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic