BAADA YA SIMBA KUELEKEA KUKAMILISHA ARENA YAKE, AZAM WATANGAZA KUFUMUA UWANJA WAO
Uongozi wa klabu ya Azam FC upo kwenye mchakato wa kukarabati kiwanja chake cha nyasi bandia ili kukiweka vizuri zaidi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffer Idd Maganga, amesema kuwa kiwanja hicho wanatajia kukifungia hivi karibuni kufanya ukarabati huo.
Maganga ameeleza wameamua kufanya maamuzi hayo ili kukiweka kwenye hadhi ya kisasa zaidi na inaonekana mechi zake za nyumbani zitakuwa zinachezewa kunako Uwanja wa Uhuru ama Taifa Dar es Salaam.
"Tutaufunga uwanja wetu wetu wa Chamazi ili kufanya ukarabati.
"Ukarabati huo utahusisha uwanja wa nyasi bandia ili kuuweka katika mandhari nzuri zaidi."
0 COMMENTS:
Post a Comment