SAID Ndemla, kiungo mshambuliaji wa Simba yupo kwenye hesabu za kocha wa Singida United Ramadhan Nswanzurimo ili akaokoe jahazi ambalo limeanza kuzama kwa sasa.
Singida United ipo nafasi ya 20 kwenye msimamo ikiwa imefunga jumla ya mabao manne pekee na imekubali kufungwa jumla ya mabao 15 ikiwa na pointi 4.
Habari kutoka ndani ya Singida zinaeleza kuwa tayari Ndemla yupo kwenye hesabu za Singida ambao wamevutiwa na uwezo wake licha ya kutopewa nafasi ndani ya Simba.
“Singida United kwa sasa hali ni tete hakuna kiungo halisi wala mshambuliaji hivyo wanampigia hesabu Ndemla ambaye anafiti kucheza nafasi ya kiungo pamoja na ushambuliaji, kinachowavutia zaidi ni ile mishuti yake ya mbali yenye nguvu,” kilieleza chanzo hicho.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana alisema kuwa mpango wa kusuka kikosi upo ila suala la nani asajiliwe lipo chini ya kocha.
0 COMMENTS:
Post a Comment