KOCHA Mkuu wa timu ya Real Madrid inayoshiriki La Liga Zinadine Zidane amesema kuwa anampenda mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe jambo lililowashtua viongozi wa timu yake.
Zidane amekiongoza kikosi chake kujikusanyoa pointi 28 kikiwa nafasi ya pili kwenye jumla ya mechi 13 za La Liga na ameshinda mechi 8 huku akilazisha sare nne na kupoteza mechi moja.
Mbappe alikuwa kwenye mpango wa kusajiliwa na Real Madrid mwanzoni mwa msimu mambo yakawa magumu kutokana na mabosi wa PSG kutokuwa tayari kuachia nyota huyo anayeshiriki Ligue 1 inayoshika nafasi ya kwanza kwenye msimamo.
Inaekezwa kuwa Mbappe yumo kwenye hesabu za Zidane kwenye usajili unaotatarajiwa kufunguliwa mwezi Januari ili akaongeze nguvu ndani ya kikosi jambo ambalo Thomas Tuchel Meneja wa PSG haamini kama litafanikiwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment