November 11, 2019


Kikosi cha Simba B jana mkoani Morogoro kimeweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kombani ya Mngeta katika muendelezo wa mechi za kirafiki wilayani Kilombero, Morogoro.

Simba B ambayo imealikwa mkoni humo na mashabiki, ilishusha kikosi chake chote kamili kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali.

Bao la Simba B liliwekwa kambani na kiungo wake fundi Cyprian John  katika dakika ya 35 ya mchezo akimalizia kanzi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji hatari Andrew Michael ambaye aliwatoka mabeki wa Kombani ya Mngeta na kupiga krosi iliyomkuta mfungaji.

Hadi dakika 45 kipindi cha kwanza Simba B ilikuwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kushambuliana kwa kasi kwa zamu lakini Simba B walikosa umakini wa kuongeza idadi ya magoli kwani kosakosa kwenye lango la Kombaini ya Mngeta zilikuwa nyingi.

Mara baada ya mechi hiyo kuisha, Kocha wa Simba B, Niko Kiondo aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo muhimu ,ambapo alisema mapungufu madogomadogo yaliyojitokeza atayafanyia kazi.

Leo kikosi cha Simba B kitashuka tena dimbani kupambana na Kombain ya Malinyi katika muendelezo wa mechi zake za kirafiki ndani ya wilaya hiyo ya Kilombero.

1 COMMENTS:

  1. Matumizi ya neno kuweza bado yana tatizo, kwenye vyombo vya habari ukishinda umeshaweza hakuna maana ya kutumia kimeweza kushinda. Inasikitisha hata kwenye mazingira hasi neno hili linatumika, utasikia watu 3 wameweza kufariki, kama vile kufariki ni kitendo cha kishujaa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic