SIMBA YAONGEZA WAWILI KIKOSINI ILI KUPATA ALAMA TATU
Kuelekea mechi ya Ligi Kuu leo dhidi ya Mbeya City, wachezaji Shomari Kapombe na Mohammed Hussein watakuwa sehemu ya kikosi cha Simba.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu timu hiyo, Mbegiji Patrick Aussems amethibitisha kwamba Kapombe na Hussein watakuwa sehemu ya mchezo baada ya kuwa fiti.
Ikumbukwe wawili hao achezaji walikosekana kwenye michezo miwili iliyopita ya Ligi Kuu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Licha ya kurejea kwao, inaelezwa straika na nahodha, John Bocco bado hali yake haijaimarika vizuri kitu ambacho kimepelekea mpaka sasa asirejee kikosini.
0 COMMENTS:
Post a Comment