November 19, 2019


Tunaweza kusema historia imeandikwa na klabu ya Simba kwa kufanikiwa kuwa na uwanja wake wa mazoezi ambao unaelekea kukamilika siku za usoni.

Simba ilianza kujenga uwanja huo miaka kadhaa iliyopita wakati wa utawala wa aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage lakini haukwenda kwa kasi kutokana na uchumi kuwa mbaya.

Uwanja huo ambao upo Bunju jijini Dar es Salaam uhusisha viwanja viwili ambapo mmoja ni wa nyasi asili na mwingine wa bandia ambavyo vyote vitatumika kwa ajili ya mazoezi.

Simba watatumia uwanja wa nyasi asili kwa ajili ya mechi ambazo watakuwa wanachezea kwenye viwanja vya mikoani na halikadhalika bandia endapo wakipangiwa kukipiga Uhuru Stadium ama Taifa, Dar es Salaam.

Ni zaidi ya miaka 80 Simba wamekuwa hawana uwanja wa mazoezi sawa na Yanga ambao nao wameanza mchakato wa kuanza kujenga.

Taarifa zilizopo ni kuwa Simba wanaweza kuanza kutumia uwanja wa Bunju mapema mwezi ujao na watakuwa wanaandika historia ya kuwa timu ya kwanza dhidi ya watani zao wa jadi Yanga kumiliki kiwanja hicho.

2 COMMENTS:

  1. Yanga wanasubiri nini kuiiga Simba katika viwanja walivyopewa kule kigamboni??? Viongozi wao siasa nyingi na kamati za kumwaga....vitendo sifuri....Wawekezaji kama Mo ni vitendo tu. Haya ya kusema wawekezaji ni wananchi kupitia kuchangishana kwenye bakuli na kuuza jezi ni kujidanganya....na ni porojo na siasa....dawa ni kutafuta mwekezaji na aanze vitendo kwa kujenga haraka haitachukua miezi 3 uwanja unatumika wakijenga usiku na mchana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama sisi Simba tulivyoiga kwa kitimu cha uchochoroni Gwambina fc ya Mwanza,Yanga jitahidini hata uwe zaidi ya ule wa Azam.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic