November 19, 2019


Baada ya kukabidhiwa eneo ambao watalitumia kujenga uwanja huko Kigambon, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka Yanga kutokuwa na haraka ya kuhamishia makazi hayo katika eneo hilo na badala yake akiwataka waendelee kuwa na subira.

Makonda ameeleza kuwa kwa sasa serikali ina mikakati kabambe ya kuhakikisha eneo la Jangwani linawekwa sawa kwanza kutokana na changamoto kadhaa zilizopo.

Ameeleza kwa kuwataka wanayanga wote wawe na subira kutokana na kiu waliyonayo lakini ahiahidi mambo yataenda vizuri kwa ajili ya kukarabati eneo hilo.

"Ndugu zangu wa Yanga msiwe na haraka.

"Msihame Jangwani kwa sasa. Serikali makini ya Rais John Magufuli italifanyia kazi eneo la Jangwani ambalo limekuwa na changamoto kwa muda mrefu na hivyo kila kitu kitaenda sawa."

4 COMMENTS:

  1. Yanga wanasubiri nini kuiiga Simba katika viwanja walivyopewa kule kigamboni??? Viongozi wao siasa nyingi na kamati za kumwaga....vitendo sifuri....Wawekezaji kama Mo ni vitendo tu. Haya ya kusema wawekezaji ni wananchi kupitia kuchangishana kwenye bakuli na kuuza jezi ni kujidanganya....na ni porojo na siasa....dawa ni kutafuta mwekezaji na aanze vitendo kwa kujenga haraka haitachukua miezi 3 uwanja unatumika wakijenga usiku na mchana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwekezaji angepatikana unadhani kuna mtu angemkataa...hata simba kama si Mo wangekywa ovyo zaidi hata ya Yanga

      Delete
    2. Kama sisi Simba tulivyoiga kwa kitimu cha uchochoroni Gwambina fc ya Mwanza,Yanga jitahidini hata uwe zaidi ya ule wa Azam.

      Delete
  2. Vyura bhana eti timu ya wananchi mwekezwji mwamanachi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic