November 16, 2019


TIMU ya Taifa ya Tanzania leo imekwea pipa kuwafuata wapinzani wao Libya mchezo wao wa pili wa kufuzu michuano ya Afcon inayotarajiwa kufanyka nchini Cameroon 2021.

Sars itamenyana na Libya nchini Tunisia ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 2-1 dhidi ya Equatorial Guinea mchezo uliochezwa jana uwanja wa Taifa.

Kwenye msafara huo nyota Erasto Nyoni ambaye ni kiraka ameachwa Bongo akipata matibabu ya goti.

Etienne Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Stars amesema kuwa ameachwa Nyoni kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata jana kwenye mchezo dhidi ya Equatorial Guinea.

5 COMMENTS:

  1. taifa stars ni kama simba sc kwa sasa, hamuachi mtu salama awapo uwanja wa taifa. hongera sana stars.

    ReplyDelete
  2. taifa stars ni kama simba sc kwa sasa, hamuachi mtu salama awapo uwanja wa taifa. hongera sana stars.

    ReplyDelete
  3. kila la kheri Stars. Tuko pamoja hadi kieleweke

    ReplyDelete
  4. Nafasi ya nyoni atacheza nani?Mkude naye vipi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic