Kufanya vizuri kwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta katika mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya timu yake Genk dhidi ya Liverpool, kumezidi kumsafi shia njia mshambuliaji huyo.
Samatta mwanzoni mwa wiki jana aliifungia Genk bao moja ilipofungwa mabao 2-1 na Liverpool kwenye uwanja wa Anfield.
Sasa Newcastle na West Ham za England zimeonyesha nia ya kumnasa mshambuliaji huyo aliyekulia Mbagala Dar es Salaam.
Samatta alisajiliwa na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Congo DR.
Kabla ya kujiunga na Mazembe alichezea Simba iliyomsajili kutoka Mbagala Market.
Samatta alikuwa mfungaji bora kwenye ligi ya Ubelgiji msimu uliopita akifunga mabao 15 na kuisaidia Genk kutwaa taji.
Kwa sasa nahodha huyo wa Stars ana mabao 13 katika kampeni za msimu huu.
Samatta alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa ndani wa Afrika mwaka 2015.
0 COMMENTS:
Post a Comment