November 3, 2019


KIKOSI cha Yanga leo kimeshindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wake Pyramids kwenye mchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho uliochezwa nchini Misri.

Yanga ilikuwa na kibarua cha kuifunga Pyramids FC mabao 2-0 ili kupenya mbele hatua ya makundi kutokana na kukubali kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba.

Licha ya jitihada za wachezaji wa Yanga kujilinda kipindi cha kwanza ngome yao ilitikiswa dakika ya 27 kupitia kwa Eric Traore kutokana na mlinda mlango kuokoa hatari iliyotua miguuni mwa mshambuliaji huyo.

Mohamed Farouk alipachika bao la pili kipindi cha pili baada ya kupigwa kona iliyomkuta na kuizamisha mazima wavuni kabla ya Abdallah El Saidj kupachika bao la tatu dakika za lala salama.

Matokeo hayo yanaitoa Yanga kwenye michuano ya kimataifa ambapo Pyramids inafuzu hatua ya makundi kwa juma ya mabao 5-1.

3 COMMENTS:

  1. ni matokeo yaliyotegemewa na wengi 98% kwa hiyo haishangazi

    ReplyDelete
  2. Wamehitahidi sana, nilifikiri angekula hamsa Leo duuuuh!? Kweli Yanga inabidi ifumuliwe haswa, kuanzia benchi la ufundi... La sivyo kiaama kinakuja ligi kuu! Zahera aende Kongo akacheze Ndombolo..!

    ReplyDelete
  3. Kumtoa Makame kulifanya beki ielemewe hata alipoingia Fei alikuwa hana ubavu na kimo cha urefu kupambana kwa mipira ya katikati, na matokeo yake Lamine na Ali Ali kutumia nguvu nyingi mwishowe kusababisha kuumia...bado benchi la ufundi limeendelea kufanya makosa kwenye substitutions...kwa mara nyingine. Kulikuwa hakuna haja ya Kumtoa Balinya timu ilishindwa kushambulia....Sadney alionekana peke yake kule mbele

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic