LEO Novemba 15 timu
ya Taifa ya Tanzania itamenyana na timu ya Taifa ya Equatorial Guinea kwenye
mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kuwania kushiriki michuano ya Afcon
inayotarajiwa kufanyika 2021.
Kwenye jumla ya mechi 4
za ushindani ambazo timu hiyo ya Taifa ya Equatorial Guinea imecheza hakuna
hata mechi moja ambayo wameambulia ushindi zaidi ya kupata sare na vichapo
wakiwa ugenini tofauti na Stars ambayo imeambulia ushindi ikiwa ugenini mbele
ya Sudan kwa kuifunga mabao 2-1.
Ilipoteza mbele ya timu
ya Taifa ya Congo kwa kufungwa bao 1-0 pia ililazimisha sare ikiwa nchini Sudan
Kusini ya kufungana bao 1-1 pamoja na ule dhidi ya Chad kwa sare ya kufungana
mabao 3-3, na iliambulia kichapo mbele ya Saudi Arabia kwa kufungwa mabao 3-2.
Kwenye jumla ya mechi nne ikiwa ugenini
imefungwa jumla ya mabao nane huku wao wakifunga mabao sita pekee.
Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya
Tanzania, Juma Mgunda amesema kuwa wanatambua ugumu wa
mchezo watapambana kupata matokeo.
“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu
tutapambana kupata matokeo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,”
amesema.








0 COMMENTS:
Post a Comment