November 6, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mshindo Msolla, umewapiga STOP viongozi wake wake Antonio Nugaz pamoja na Fredrick Mwakalebela juu ya kuzungumza na vyombo vya habari, imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa, Mwakalebela ambaye ni Makamu Mwenyekiti Yanga, amepewa onyo hilo ili kuacha kupasha taarifa ambazo zinakuwa hazijajadiliwa katika kamati ya utendaji ya klabu.

Mbali na Mwakalebela, aidha taarifa imeeleza kuwa Msolla amemzuia pia Ofisa Mhamasishaji Antoni Nugaz kuzungumza vitu ambavyo havina maana na vyombo vya habari mara kwa mara.

Msolla ameamua kutoa kauli hiyo ili kuwapunguzia kasi wawili hao na akiwataka watoa taarifa kwa taratibu maalum za klabu kama ilivyo ada.

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic