NOEL
Mwandila, Kocha Msaidizi wa timu ya Yanga amesema kuwa wana matumaini ya kufanya vizuri kesho mbele ya Prymids baada ya kutambua makosa yao kwenye mchezo wa kwanza jambo watakaloliepuka kwenye mchezo wa marudio
wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Novemba 3.
Kwenye
mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba Yanga ilikubali kufungwa
mabao 2-1 na Pyramids hivyo ili kusonga mbele watahitaji mabao 2-0 ugenini.
Mwandila
amesema kuwa mpira wa sasa umebadilika tofauti na zamani jambo linalowapa nguvu
ya kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa marudio.
“Tulizidiwa
mbinu kipindi cha kwanza hilo lipo wazi ila kipindi cha pili tulibadilika na
timu ilicheza mpira ambao ulionekana na kila shabiki, kwa kuwa tumefungwa
tunajiaanda kushinda kwao hakuna jambo jingine.
“Hakuna
darasa la kukata tamaa kwenye mchezo wa mpira jambo linalotufanya tuamini
kwamba nasi tutashinda, lengo letu ni moja kuwafuata wapinzani wetu kishujaa na
si kinyonge kwani wanafungika,” amesema Mwandila.
0 COMMENTS:
Post a Comment