November 17, 2019


YANGA leo imeibuka na ushindi mbele ya Coastal Union kwa ushindi wa mabao 3-1 mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa.

Coastal Union ilianza kupata bao la kwanza dakika 44 alilojifunga Ally Mtoni 'Sonso'  akimalizia pasi ya Mudhatir lililowapleka  Yanga kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa nyuma kwa bao 1.

Kipindi cha pili Yanga iliyo chini ya Boniface Mkwasa ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Mussa nafasi yake ikachukuliwa na Ngassa.

Ngassa alifungua pazi la mabao dakika ya 69 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 lililomuacha mlinda mlango akiwa hana namna ya kufanya.

Dakika 90+1 Pappy Tshishimbi alipachika bao la pili lililowafanya Yanga kuwa mbele kwa mabao mawili kabla ya Balinya kuandika bao la tatu la ushindi dakika ya 90+4 kwa mkwaju wa penalti.

Boniface Mkwasa, kaimu kocha wa Yanga amesema kuwa mwelekeo kwa wachezaji umeanza kuonekana na kila mchezaji anaonyesha ile alichonacho.

1 COMMENTS:

  1. Nimeangalia mechi ya leo,nionavyomimi ni vizuri kumpuzisha Molinga iliwacheze watu wengine

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic