November 29, 2019


Kikosi cha Yanga leo Novemba 28, 2019 kitacheza dhidi ya Alliance ya jijini Mwanza mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku ikiwakosa baadhi ya wachezaji ambao ni majeruhi na waliotwa katika timu ya taifa ya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wachezaji wanne walioitwa katika Timu ya taifa ya Zanzibar wamewaacha akiwemo Ally Ally , Abdulaizi Makame, Feisal Salum na Mohammed Issa huku Mapinduzi Balama akiwa majeruhi aliyopata katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania huku wachezaji wengine wakiwa wapo tayari kwaajili ya mchezo huo.

Aidha Afisa Muhasishaji wa klabu ya Yanga, Antonio Nugaz ametoa ratiba ya shughuli za kijamii ambazo zitafanyika kesho asubuhi kabla ya mechi hiyo ikiwemo kutembelea katika hospitali ya Bugando pamoja na viongozi watakaokuwa nao katika shughuli hiyo.

Yanga itashuka katika dimba la CCM kirumba jijini Mwanza Kesho Novemba 29 dhidi ya Alliance ambao wametoka kupigwa mabao 5-0 na Azam FC katika uwanja wao wa Nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic