December 8, 2019


Ukichana na wachezaji watatu waliokuwa wametajwa hapo awali, inaelezwa pia kuwa Mnamibia Sadney Urikhob naye ameandika barua ya kuachana na Yanga.

Sekeseke la wachezaji wengi wa kigeni Yanga kuondoka limezidi kushika kasi baada ya kuelezwa kuwa David Molinga, Juma Balinya na Lamine Moro kuanzisha suala hilo.

Maamuzi ya wachezaji hao yamekuja kufuatia kudai stahiki zao ambazo ni fedha za mishahara za miezi kadhaa ambazo hazijatolewa mpaka sasa.

Wachezaji hao wa kigeni kwa mujibu wa taarifa wameshindwa kuvumilia kiasi cha kwamba imewapelekea kuandika barua ili waondoke kwa ajili ya kutafuta maisha sehemu zingine.


4 COMMENTS:

  1. Hao ni machipukizi ya zahera yaondoke tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Januari nne itatoa matokeo sahihi ikiwa siasa zitaendelea na mishahara haitalipwa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic