Ukichana na wachezaji watatu waliokuwa wametajwa hapo awali, inaelezwa pia kuwa Mnamibia Sadney Urikhob naye ameandika barua ya kuachana na Yanga.
Sekeseke la wachezaji wengi wa kigeni Yanga kuondoka limezidi kushika kasi baada ya kuelezwa kuwa David Molinga, Juma Balinya na Lamine Moro kuanzisha suala hilo.
Maamuzi ya wachezaji hao yamekuja kufuatia kudai stahiki zao ambazo ni fedha za mishahara za miezi kadhaa ambazo hazijatolewa mpaka sasa.
Wachezaji hao wa kigeni kwa mujibu wa taarifa wameshindwa kuvumilia kiasi cha kwamba imewapelekea kuandika barua ili waondoke kwa ajili ya kutafuta maisha sehemu zingine.








Ndio tutamiliki kiwanja Hivo?
ReplyDeleteBado Yanga imekosa kiongozi mbunifu aisee
ReplyDeleteHao ni machipukizi ya zahera yaondoke tu
ReplyDeleteJanuari nne itatoa matokeo sahihi ikiwa siasa zitaendelea na mishahara haitalipwa
Delete