December 14, 2019


Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yessayah ‘AY’ ameiangukia Serikali, makampuni na watu binafsi akiwasihi kuwekeza zaidi kwenye tuzo za muziki nchini.

AY alizungumza hayo jana kwenye mahojiano maalum kupitia Kipindi cha Bongo 255 kinachorushwa na +255 Global Radio.

AY alisema tuzo hizo zitakuwa ni chachu kwa wasanii kutengeneza muziki mzuri zaidi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Tuzo zinaleta hamasa na ushindani, wadau kuanzia Serikali, makampuni na watu binafsi wanapaswa kuona fursa hii.

Pia aliwataka wasanii kwenda nje ya nchi na kufanya muziki wa kimataifa ili kupata ladha mpya na kubadilishana uzoefu na wasanii wakubwa duniani.

Mkali huyo wa Rap ameachia video ya ngoma mpya iitwayo Distance Remix ambayo amefanya na Jay Rox wa Kenya pamoja na msanii kutoka WCB, Rayvanny.

AY amesema aliisikia ngoma hiyo ikipigwa wakati akiwa kwenye harakati zake, hivyo akaipenda na kufanya mawasiliano na msanii aliyeimba ngoma hiyo, Jay Rox ambaye alikubali hivyo wakaingia studio na kuifanya upya.

“Nilikuwa na malengo ya kufanya ngoma kali na kuiachia kabla ya mwaka huu haujaisha, namshukuru Mungu nimefanikiwa na Distance Remix ambayo ina wiki moja sasa inafanya vizuri kwenye platforms mbalimbali za muziki,” amesema AY.

Video ya Distance Remix hiyo imeandaliwa na Director Kenny, mixer amefanya Paul Kruz na producer ni Kenz Ville Marley.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic