AZAM FC jana imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya kikosi cha Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa hisani ya kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu hizo mbili Ibrahim Jeba.
Mchezo huo ulichezwa majira ya saa 2:00 usiku visiwani Zanzibar ulitanguliwa na dua maalumu ya kumuombea kheri Jeba aliyefariki mwaka huu 2019.
Mabao ya Azam FC yalipatikana kupitia Kwa Obrey Chirwa dakika ya 27 alifunga kwa mkwaju wa penalti baada ya Stamili Mbonde wa Mtibwa Sugar kunawa mpira ndani ya 18.
Bao la pili Kwa Azam FC lilipachikwa dakika ya 54 kupitia kwa kiungo wao Djodi akimalizia pasi ya Bruce Kangwa.
Kwenye mchezo huo wa hisani kulikuwa na jezi maalumu za Jeba ambazo zilikuwa na jina la Jeba huku wachezaji wa Mtibwa walivaa jezi namba 22 aliyokuwa anaivaa Jeba enzi za uhai alipokuwa akikipiga Mtibwa Sugar.







0 COMMENTS:
Post a Comment