December 13, 2019


Aliyekuwa straika wa Yanga, Juma Balinya, amesema ameondoka Tanzania na akiamini ipo siku atarejea tena. Imeelezwa.

Balinya ambaye alisajiliwa kabla ya msimu huu kuanza, ameichezea Yanga takribani mechi saba pekee kabla ya kuvunja mkataba wake.

Balinya ameeleza kuwa anaondoka Tanzania lakini ipo siku atarejea sababu maisha ya mpira ni popote.

"Huu ni mpira, naondoka lakini naamini ipo siku nitarejea," alisema.

Mashabiki Simba wanasemaje

Baada ya kuondoka kwa Balinya pale Yanga, baadhi ya mashabiki Simba wamesema endapo mchezaji huyo atatua kwao kuna uwezekano akang'ara zaidi.

Baadhi yao wameeleza kuwa Yanga hakupewa na nafasi na kutokana na kung'ara Uganda kabla hajatua Jangwani wanaamini anaweza akafunga zaidi akipata nafasi ya kucheza na Meddie Kagere.

8 COMMENTS:

  1. Huyu tayari Simba wamemrubuni wakisaidiwa na Msola "mark my words"...Muda hakimu mzuri mtayasikia!

    ReplyDelete
  2. Vipi atarajiwe Balinya acheze kwa ufanisi Yanga na kutia maguli na huku Bila ya kulipwa chake. Hugo atatuwa Simba kwa ari kubwa na kuyafanya tale aliyoshindwa kuyafanya pale JangWani

    ReplyDelete
  3. Kwani Simba ndo walikuwa wanapanga kikosi cha Yanga? Jamani hebu tujaribu kuwa wakweli kuliko kuwahadaa mashabiki ambao kila siku ndoto zao ni ushindi. Tuwe wa kweli na ukweli kuhusu timu yetu ya Yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna visingizio dhaifu na kutaka kuwafanya mashabiki na wanachama kwamba hawana kumbukumbu na yanayoendelea. Zile mbwembwe za kumtambulisha kwenye KUBWA KULIKO zimeishia sasa kusema anarubuniwa na simba kana kwamba alishacheza mechi nao!! January 4 Dr. Msola na genge lake nadhani watajifunza kitu

      Delete
  4. ki ukwel mimi ni shabiki damu wa nyanga ila tarehe 4 tunapakatwa msolla kmamaee

    ReplyDelete
  5. Yanga wamekua kama vyura waliozidiwa na mvua ya mafuriko jangwani ila hawataki kujisalimisha kuomba msaada.

    ReplyDelete
  6. Yaani eti Simba wamrubuni balinya kwa kipi cha ziada alichonacho, shughulikieni kilichomwondoa na kusingizia Simba, zile mbwembwe za kumtambulisha sizioni saiz!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic