December 18, 2019


Kama mambo yataenda vizuri basi mlinzi wa pembeni wa Yanga, Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye amekuwa nje kwa kitambo kidogo anaweza kuibukia kwenye mechi dhidi ya Simba, Januari 4, mwakani baada ya kuanza mazoezi madogo madogo.

Boxer hadi sasa amecheza mechi moja tu ya Yanga msimu huu ambapo amekuwa nje kutokana na tatizo la goti ambalo limemuweka nje kwa muda wote huo.

“Namshukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri, naendelea na matibabu ya majeraha yangu ambapo napatiwa matibabu mazuri sana.

“Nishaanza mazoezi madogo madogo kwa kipindi hiki na niwajulishe kwamba siku si nyingi nitarudi uwanjani kwa mara nyingine kwa sababu naendelea vizuri kwa sasa,” alisema Boxer.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic