Kipa wa zamani wa Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiweka sokoni katika usajili wa dirisha dogo kwa kuzikaribisha timu ambazo zitamuhitaji.
Dida ambaye kwa sasa anajishughulisha na kilimo, aliachwa na Simba katika usajili uliopita, kwa sasa anahitaji timu ya kuitumikia.
Usajili wa dirisha dogo unatarajiwa kufunguliwa Desemba 16, ambapo Dida amesema: “Hakuna timu iliyonifuata hadi sasa kuhitaji huduma yangu nadhani muda bado haujafi ka na dirisha likifunguliwa nina imani kuna timu ambazo zitanifuata.
“Nipo tayari kutua timu yoyote ile itakayonihitaji niweze kuitumikia msimu ujao, kwani nipo fiti na ninaendelea na mazoezi binafsi ya kujifua na nikipata timu naamini nitaitumikia vyema.”
0 COMMENTS:
Post a Comment