STARS YATUPWA NJE CECAFA NA UGANDA, YACHAPWA 1-0
Kikosi cha Taifa Stars kimeondolewa katika michuano ya CECAFA baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Uganda.
Stars imeondolewa katika michuano hiyo ambayo ilikuwa inafanyika nchini Uganda kwa bao pekee ambalo limewekwa kimiani na Fahad Bayo mnamo dakika ya 86.
Katika mchezo huo Stars ilishuhudiwa kipa wake Aishi Manula akiumia na kutolewa nje kwa machela na kusababisha nafasi yake ichukuliwe na Metacha Mnata.
Baada ya kutolewa, Stars sasa inaweza ikaanza safari ya kurejea nchini kati ya kesho ama keshokutwa.
Tuwe wa kweli kabisa licha ya kuahidiwa zawadi nono vijana wetu kama wangebeba kombe kwenye mashindano haya lakini wameshindwa kufikia malengo. Kwa watanzania kama kawaida yetu ni watu wa siasa sana hapana shaka sifa zitamwagika sana kuwa Taifa stars imefanya vizuri na wachezaji wanastaili pongezi. Hizi kauli hujirejea kila mara pale timu yetu ya Taifa zetu zinapofanya vibaya. Kama ni mgonjwa basi Taifa stars ni mgonjwa anaekwenda hospitali kupima afya yake lakini kila anapopima afya yake haonekani kuimarika kifya ila watu wake wanazidi kumsifia kuwa anafanya vizuri? Amejipima vizuri blah blah ila hali ya mgonjwa huo bado ni tete na dhaifu. Ninachotaka kusema ni kwamba Dunia hii ya leo kila kitu ni vita lakini sisi watanzania tunachukulia kila poa. Iwe uchumi,iwe elimu,iwe afya,iwe michezo,iwe mapenzi ukifanya kwa mazoea bila yakuwa na nia ya dhati yakuwa the best basi utakuwa mtu wa kujiliwaza kwa siasa kila siku huku ukiwamodolea nacho watu wakichukiwa unachokitaka. Waganda wanakitu kinachoitwa fighting spirit yaani moyo wa kupambana iwe ugenini au nyumbani.
ReplyDeleteWatanzania laziama kuna sehemu tunakosea na tusipokaa chini tukatafakari basi katika sekta ya michezo hatuwezi kutoka. Kuna wakati najiuliza sana kama wazo la Muheshimiwa Magufuli la kuwa na JKT maalum ya soka kwa vijana wadogo wenye vipaji.Najiuliza kama angalau kama wahusika walikaa chini na kutafakari wazo hilo. Tuache chuki na siasa Magufuli is gifted person na kauli zake nyingi za kujenga kitu fulani si za, kuziacha zipite hivi hivi kama si uzembe kwa wahusika. Yaani kuwe na JKT ya soka,vijana wakiifunzwa si mpira tu bali uzalendo pia wa kulipiania taifa.