December 5, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa nahodha wa kikosi hicho John Bocco yupo tayari kwa ajili ya mapambano baada ya kuwa fiti kwa asilimaia mia.

Bocco alipata majeraha ya goti kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC uwanja wa Taifa alikwea pipa mpaka Afrika Kusini hivi karibuni kufanyiwa vipimo.

Akizungumza na Saleh Jembe, meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwa sasa Bocco anaendelea vizuri na ameanza kufanya mazoezi na wenzake.

"Bocco amerejea nchini anafanya  mazoezi na wenzake. Majibu ya Afrika Kusini baada ya kufanyiwa vipimo ni kwamba anaendelelea vizuri.

"Ikiwa mchezaji anafanya mazoezi na wenzake maana yake yupo fiti hivyo ni suala la kusubiri kuona itakuaje," amesema.

Mchezo wa kwanza wa Simba mwezi Januari 4 itakuwa dhidi ya Yanga kuna uwezekano akaiwahi mechi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic