AZAM FC iliyo chini ya Arstica Cioaba ambao ni Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), Azam FC, wamepania kupata matokeo mbele ya African Lyon kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya michuano hiyo utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex kati ya Desemba 22 na 28 mwaka huu.
Azam FC ilitwaa taji hilo msimu uliopita mbele ya Lipuli ya kwa ushindi wa bao 1-0, lililowekwa kimiani na Obrey Chirwa na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Kikosi cha Azam FC kitarejea mazoezini leo Alhamisi jioni baada ya wachezaji kumaliza mapumziko ya siku tatu waliyopewa.







0 COMMENTS:
Post a Comment