DAKIKA ya 25, Cristiano Ronaldo mshambuliaji wa Juventus aliamsha hasira za timu ya Lazio baada ya kuwa wa kwanza kupachika bao kwenye mchezo huo wa Seria A.
Lazio ilizinduka baada ya dakika 10 na kufunga bao la kwanza dakika ya 45+1 kupitia kwa Luiz Felipe Ramos Marchi na kufanya waende kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ngoma ikiwa 1-1.
Kipindi cha pili Lazio ilichangamka na kuandika bao la pili dakika ya 74 kupitia kwa Sergej Milkovic-Savic na bao la tatu likipachikwa na Felipe Caicedo dakika 90+5 na kufanya ishinde mabao 3-1 mbele ya Juventus.
Mchezo huo ulishuhudia kadi nyekundu kwa nyota wa Juventus, Juan Cuardrado dakika ya 69.
Matokeo hayo yanaifanya Juventus kupoteza mechi moja kati ya 15 ilizocheza ikiwa nafasi ya pili na pointi 36 huku Lazio ikiwa nafasi ya tatu ina pointi 33 imepoteza mechi mbili baada ya kucheza mechi 15.
Kinara ni Inter Milan mwenyewe ana pointi 38 kwenye mechi 15 amepoteza moja pia.








0 COMMENTS:
Post a Comment